#SheriaYaLeo (84/366); Akili kama msuli.
Akili zetu huwa zipo kama msuli.
Msuli unapotumika unakua na kuimarika.
Na msuli usipotumika unasinyaa na kuwa dhaifu.
Akili ikitumika inakua na kuimarika na isipotumika inasinyaa na kuwa dhaifu.
Kinachofanya akili isinyae isipotumika ni mambo mawili.
Moja ni kupenda mazoea. Tukishakuwa na fikra au njia fulani ya kufanya kitu, huwa tunaendelea na hiyo kwa muda mrefu. Hatupendi kujihangaisha na mambo mapya na yasiyo na uhakika. Kwenda na mazoea hakuikuzi akili.
Mbili ni tabia ya akili kukimbia mambo magumu. Akili huwa haipendi kutumia nguvu zake kama hakuna umuhimu mkubwa. Hivyo huwa inatafuta njia rahisi kwenye jambo lolote lile. Usipoilazimisha akili ikae kwenye jambo gumu, italikimbia jambo hilo na hivyo haiwezi kukua na kuimarika.
Njia pekee ya kuepuka hayo ni kuilazimisha akili kufikiri kwa utofauti.
Hapo ndipo unapoweza kupata mawazo ya kibunifu na kuiwezesha akili yako kukua na kuimarika zaidi.
Ichangamshe akili yako kupitia utofauti ili uweze kuibua ubunifu mkubwa ulio ndani yako.
Sheria ya leo; Usikubali kukaa kwenye mazoea. Ilazimishe akili yako kufikiri vitu tofauti. Jifunze vitu usivyovijua. Fikiria mambo ambayo huna uelewa nayo. Tumia kila njia kuichangamsha akili ili uibue ubunifu na uweze kuikuza pia.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji