#SheriaYaLeo (99/366); Tawala hisia zako.
Watu wenye hasira huwa wanaishia kudharauliwa na kuonekana hawana maana kwa sababu hisia zao huwa haziendani na kile kilichotokea.
Hasira huwafanya watu wafanye mambo ambayo baadaye huja kuyajutia.
Wanayapa mambo uzito uliopitiliza na hatimaye kujibu kwa kupitiliza.
Wengi huona hasira ni sifa na kiashiria cha mamlaka.
Lakini watu ni rahisi kuwadharau wenye hasira na kujua hawana mamlaka yoyote.
Watu wakishajua una hasira za haraka, wanakutega uingie kwenye hasira ili ufanye maamuzi ambayo ni mabovu kwako na yenye manufaa kwao.
Katika safari yako ya mafanikio na maisha kwa ujumla, tawala sana hisia zako.
Usionyeshe waziwazi hisia zako kwa namna ambayo watu wanaweza kuzitumia kwa kujinufaisha wao wenyewe.
Sheria ya leo; Kuonyesha hasira na hisia nyingine ni ishara ya udhaifu. Kama huwezi kujidhibiti mwenyewe kwenye hisia zako, utaweza kudhibiti kitu gani?
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji