#SheriaYaLeo (100/366); Linda Sifa Yako.
Sifa yako ni eneo muhimu sana la maisha yako.
Unaweza kupata au kukosa fursa mbalimbali kutokana na sifa uliyonayo.
Watu watakuchukulia kulingana na sifa uliyonayo.
Kukuheshimu au kukudharau kutatokana na sifa yako.
Katika safari yako ya mafanikio, ni muhimu sana kujenga na kulinda sifa yako.
Sifa yako iweze kuwa na ushawishi mkubwa kwa watu ili wawe tayari kukupa kile unachotaka.
Katika mambo yote kwenye maisha, kubomoa ni rahisi kuliko kujenga.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye sifa yako.
Unaweza kujijengea sifa kwa miaka 20, halafu ukaja kuivunja ndani ya sekunde 20.
Ukishabomoa sifa yako ni vigumu sana kuijenga tena. Kwani watu hawatakuamini tena kirahisi.
Na wapinzani au washindani wako watatumia hilo kukuangusha zaidi.
Ni kwa sababu hizo ndiyo kujenga na kulinda sifa yako ni wajibu mkubwa na muhimu sana kwako.
Usiuchukulie kirahisi, badala yake upe uzito unaostahili.
Sheria ya leo; Sifa ndiyo msingi mkuu wa mamlaka na mafanikio. Kupitia sifa unaweza kushawishi na kushinda mambo mbalimbali. Pale inapoharibika inakuwa kikwazo kwako kupata unachotaka. Jenga na linda sana sifa yako, umuhimu wake ni mkubwa kwako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji