#SheriaYaLeo (107/366); Usichukue upande wowote.
Sisi binadamu kama viumbe wa kijamii, huwa tunapenda kuwa ndani ya kundi na hivyo huwa tunakimbilia kuchukua upande fulani katika pande zinazokuwepo.
Lakini hilo huishia kukunyima wewe nguvu na fursa za kufanya makubwa zaidi.
Unapochukua upande mmoja na watu wakaona wanakumiliki, wanakuchukulia kawaida.
Unakuwa mtumwa kwao na kulazimika kufanya yale wanayotaka wao.
Lakini unapoacha kuchukua upande wowote na kusimama wewe mwenyewe, kila upande utakuwa unakazana kukushawishi uchague huo.
Hilo linakupa wewe nguvu na fursa za kufanya makubwa zaidi.
Unapoacha kuchagua upande na kusimama mwenyewe, watu wanashindwa kukuelewa na hilo linawafanya wakuheshimu zaidi.
Unapokimbilia kuchagua upande watu wanakuelewa na kukudharau.
Usichague upande wowote, usikubali umilikiwe na yeyote au kundi lolote.
Badala yake simama imara ukijitegemea mwenyewe na hilo litafanya kila upande ukuheshimu ili kukushawishi ujiunge nao.
Na usidanganyike kwamba ukikubali ndiyo watakuheshimu zaidi, heshima inakuwepo pale ambapo watu bado hawajakumiliki.
Sheria ya leo; Usikimbilie kujiweka kwenye upande wowote. Wape watu matumaini kwamba unaweza kujiunga na upande wao ili kila upande uendelee kukushawishi na kukuheshimu, lakini usichague upande wowote.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji