#SheriaYaLeo (110/366); Sifia kwa umakini.

Njia nzuri ya kukubalika na wale walio juu yako ili wakupe fursa nzuri za kupata kile unachotaka ni kuwasifia.

Sisi binadamu huwa tunapenda sana kusifiwa, inatufanya tujione ni wa muhimu sana.

Lakini unapaswa kuwa makini sana kwenye kusifia kwako, kwani ni rahisi mtu kuona unamsifia ili kupata unachotaka.

Njia bora ya kufanya hivyo ni kusifia kusiko kwa moja kwa moja na kusifia kile ambacho wengine hawasifii.

Watu wengi huwa na sifa ambazo wanazijali sana ila hakuna wengi wanaozisifia.
Wewe ukizijua sifa hizo na kuwasifia nazo, utajenga ushawishi kwao.

Katika safari yako ya mafanikio unahitaji kuwa na ushawishi mkubwa kwa walio juu yako.
Kwa kuwa watu hao tayari wamekuzidi kwa mengi, kitu pekee unachoweza kuwapa kikawa na ushawishi ni kuwasifia.

Bado binadamu ni wadhaifu kwenye eneo hilo hivyo unapomsifia mtu, unakuwa kama umemfunga kwenye eneo ulilomsifia, atataka aendelee kuonekana hivyo hivyo.
Unapaswa kusifia kwa umakini na kwa namna ambayo inakusaidia wewe kupata kile unachotaka.

Sheria ya leo; Kusifia kunaweza kufanya maajabu makubwa, ila kuna hatari zake. Ukionekana unasifia ili upate unachotaka inaharibu kabisa. Kisifia kusiko kwa moja kwa moja na kusifia yale ambayo hayasifiwi na mengi kuna nguvu zaidi.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji