#SheriaYaLeo (111/366); Watu wanakuchukulia vile unavyojiweka.

Jinsi unavyojiweka ndivyo watu wanavyokuchukulia.
Kama unajithamini na kujiheshimu, watu pia watakuthamini na kukuheshimu.

Kama unajidharau na kutokujithamini, hivyo pia ndivyo watu watakavyokuchukulia.

Ukijiweka wa kawaida na wa bei rahisi, hivyo ndivyo watu watakavyokuchukulia, kwa ukawaida kabisa.

Wote wanaoheshimiwa sana na kuthaminiwa ni kwa sababu wamejiwekea viwango vya juu na kutokukubali kushuka chini ya viwango hivyo.

Ni juu yako kuchagua viwango vyako.
Ni wewe wa kujiwekea bei yako.
Huwezi kupata zaidi kama hutataka zaidi.
Na hata kama watu hawatakupa kile kikubwa unachotaka, watakuheshimu kwa namna unavyojithamini.

Na kadiri watu wanavyokuheshimu kutokana na viwango vyako vya juu uliyojiwekea, ndivyo unavyokuwa kwenye nafasi ya kupata fursa nzuri zaidi.

Sheria ya leo; Kwa kujiamini na kujijeshimu unawafanya wengine nao wakuamini na kukuheshimu kitu kinachokupa fursa nzuri za kupata unachotaka.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji