2613; Sasa na baadaye.
Chochote kinachokulipa vizuri sasa, hakitakulipa vizuri baadaye.
Chochote kinachokupa raha sasa, kitakuumiza baadaye.
Ni kitu kinachoweza kuonekana ni kigumu, lakini ndivyo asili ilivyo.
Vizuri huwa haviambatani kwa pamoja
Kupata kimoja lazima uwe tayari kupoteza kingine.
Kitu ambacho ni tofauti kabisa na asili yetu binadamu.
Ambao huwa tunafikiria zaidi sasa kuliko baadaye.
Haishangazi kwa nini wanaofanikiwa ni wachache sana.
Kwa sababu ndiyo wanaoweza kwenda kinyume na asili yetu binadamu.
Na raha, kila mtu anaitaka sasa bila kujali kesho.
Inahitaji roho ngumu ukatae raha ya sasa ili kupata kubwa zaidi baadaye.
Na ndiyo maana waliofanikiwa wakati mwingine huonekana ni wenye roho mbaya na wasiojali.
Wanajua kujiendekeza wao wenyewe na hata wengine haijawahi kuwa njia nzuri ya kufanikiwa.
Hatua ya kuchukua;
Kabla ya kukimbilia chochote kizuri kwa sasa, jiulize kinakuzuia kupata kipi bora zaidi baadaye.
Jua chochote unachokubali sasa, umekataa kingine kwa baadaye.
Hivyo hakikisha unaweka mazingira ya kupata makubwa na bora zaidi baadaye.
Tafakari;
Kwa watu wa kawaida, roho mbaya ni kujiendekeza na kuendekeza wengine. Ndiyo maana walioshindwa huwaona waliofanikiwa wana roho mbaya.
Usiangalie sana wengine wanasemaje au kukuchukuliaje, wewe fanya kile kilicho sahihi kulingana na unachotaka.
Kocha.