#SheriaYaLeo (119/366); Kupuuza ni kisasi bora.

Pale tunapofanya makosa, halafu tukatumia nguvu kubwa kutaka kuyaondoa au kuyaficha, huwa tunatengeneza makosa makubwa zaidi.

Pale watu wanapotukosea, halafu tukapanga kulipa kisasi, tunafanya mambo kuwa makubwa zaidi.

Namna bora ya kushughulika na makosa yako au kulipa kisasi, hasa kwa mambo yanayohusisha wengine ni kupuuza.

Chukulia ni jambo dogo na lisilokuwa na nguvu au umuhimu wowote.
Endelea na maisha yako na shughuli zako kama vile hakuna kilichotokea.

Kwa namna hiyo, jambo linakosa nguvu na kupiga, huku wewe ukibaki imara.

Watu wengi wamekua wanayakuza matatizo kwa kukazana kuyatatua au kuyaficha.
Nenda kinyume na hilo, yapuuze na hayatakusumbua kwa namna yoyote ile.

Sheria ya leo; Kadiri unavyokazana kuyatatua au kuyaficha makosa yako ndivyo unavyoyafanya kuwa makubwa na mabaya zaidi. Yapuuze na yatakosa nguvu na kupotea.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji