2616; Ni rahisi kwa wengine.
Ukiwa unaona watu wengine wanafanya vitu, unaweza kuona ni rahisi.
Ni mpaka pale unapoingia mwenyewe kufanya ndiyo unajua ni vigumu kiasi gani kufanya.
Unapoona mwingine anakwama kufanya maamuzi au kuchukua hatua fulani unaweza kuona ni rahisi na wanajiendekeza, lakini unapokuwa kwenye nafasi hiyo unaona ilivyo vigumu kufanya hivyo.
Ni rahisi kushauri watu wafanye vitu fulani pale ambapo wewe huhusiki kufanya moja kwa moja.
Lakini unapohusika kufanya, unagundua jinsi gani kuna ugumu.
Hatua ya kuchukua;
Usidharau kitu chochote ambacho hujakielewa kwa undani.
Usidanganyike na yale unayoona kwa nje au kuyasikia.
Yaliyo ndani huwa ni tofauti kabisa.
Hivyo hakikisha unajitoa kweli kwenye kitu kama unataka kukikamilisha kweli.
Tafakari;
Unapoona kitu ni rahisi kwa kuangalia kwa nje, jua huo siyo uhalisia.
Ndani vitu huwa ni tofauti kabisa na vinavyoonekana kwa nje.
Jua hili mara zote ili usijidanganye na kujihadaa.
Kocha.