#SheriaYaLeo (120/366); Usitabirike.
Watu huwa wanajaribu kusoma sababu iliyo nyuma ya kila hatua unayochukua.
Ukiwa mtu wa kuchukua hatua kwa namna fulani na sababu zinazoeleweka, unatabirika kirahisi.
Na watu wakishaweza kukutabiri, wanakutawala kirahisi.
Sisi binadamu ni viumbe wa kitabia, huwa tunafanya yale tuliyozoea kufanya na hilo linapelekea tutabirike kirahisi.
Mara kwa mara chukua hatua ambazo zinawavuruga watu na kuwafanya washindwe kukutabiri.
Wasiweze kuelewa sababu ya wewe kufanya kile unachofanya.
Kwa kufanya hivyo, unawaweka watu kwenye hali ya kukufuatilia kwa umakini zaidi, kutaka kukusoma ili kuweza kukutabiri.
Kwa kuwa utaendelea kutokutabirika, unakuwa umewadhibiti watu hao.
Kadiri unavyofanikiwa ndivyo kutabirika kwako kunakuwa mzigo kwako.
Watu watakuhadaa kwa mazoea yako na kujinufaisha kwa namna wanavyotaka wao wenyewe.
Hivyo hakikisha hutabiriki kirahisi, wafanya watu waweke umakini mkubwa kwako na siyo kukuchukulia kwa mazoea.
Sheria ya leo; Kadiri usivyotabirika kirahisi ndivyo watu wanavyokuheshimu zaidi. Ni wale wa kawaida pekee ndiyo wanaotabirika kirahisi, wanaofanikiwa sana huwa hawatabiriki.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji