#SheriaYaLeo (126/366); Kuwa makini na watu unaowachokoza.

Watu huwa wanabadilika, hakuna anayebaki pale alipoanzia.
Mtu anaweza kuwa chini leo, lakini siku zijazo akawa juu kabisa.

Hivyo kuwa makini sana na watu unaowachokoza, kuwadharau au kuwatukana.
Leo anaweza asiwe na nguvu ya kukufanya chochote, lakini siku zijazo akawa na nguvu na akalipa kisasi.

Watu huwa wanasahau mambo mengi kwenye maisha yao, ila kamwe hawasahau pale wanapotendewa vibaya, kwa kutukanwa, kudharauliwa na kuumizwa.

Watu watabeba vinyongo vyao kwa muda mrefu na pale wanapokuja kupata fursa, wanafanya malipizi.

Ni vyema kumheshimu kila mtu hata kama anaonekana yuko chini kiasi gani.
Maana hujui kesho yeye atakuwa wapi na wewe utakuwa wapi.

Hakuna unachopoteza kwa kumheshimu kila mtu.
Bali una mengi ya kupata na kuepuka, utaepuka kutengeneza maadui wasio na tija.

Hata kama upo juu kiasi gani, usimdharau yeyote hata aliye chini kiasi gani.
Mambo hubadilika na watu hawasahau wanapoumizwa.

Sheria ya leo; Ondokana na msukumo wa kudharau au kuumiza wengine kwa sababu wako chini yako kwa sasa. Mambo hubadilika na hatari ya uliowaumiza kuja kulipa kisasi ni kubwa kuliko raha unayopata kwa kuwaumiza sasa.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji