#SheriaZaLeo (127/366); Unachoona siyo uhalisia.

Watu huwa wanatumia mwonekano wa nje kuwahadaa wengine.
Pale wanapokuwa na udhaifu fulani, huwa wanatengeneza mwonekano unaoficha udhaifu huo.

Lengo lao ni kuwanasa wengine kwa namna ambayo wao watanufaika zaidi.

Wewe kuwa makini usinase kwenye mitego huo.
Jua siyo kila unachoona kwa nje ndiyo uhalisia wenyewe.

Badala yake jua kuna uwezekano mkubwa kwamba mtu anakuonyesha kile anachotaka uone ili kukushawishi kwa namna fulani.

Unapokabiliana na watu wengine, chunguza ukweli wa ndani yao na siyo kuhadaika na kile wanachokuonyesha kwa nje.

Unapoona mtu anatumia nguvu kubwa kutengeneza mwonekano fulani wa nje, jua ndani uhalisia ni kinyume chake.

Hilo litakusaidia usinase kwenye mitego ambayo wengine wamekuwekea ili wajinufaishe wao zaidi.

Sheria ya leo; Kamwe usichukulie mwonekano wa nje kama ndiyo uhalisia. Jua wengi wanaigiza ili kukamilisha yale wanayotaka.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji