2627; Ugumu wa kufanya maamuzi.
Mara nyingi watu hushindwa kufanya maamuzi kwa sababu hawataki kupoteza chochote.
Wanataka wale pipi halafu wabaki nayo pia.
Kitu ambacho hakipo.
Ni labda ule pipi, upate utamu ila usiwe nayo tena.
Au usile pipi hiyo, ukose utamu ila ubaki nayo.
Kila maamuzi unayofanya, kuna kitu unapata na kuna kitu unapoteza.
Hakuna maamuzi ambayo unapata tu bila kupoteza, au kupoteza tu bila kupata.
Hivyo eneo la kufanyia maamuzi siyo kuangalia kutokupoteza, bali kuangalia kupata ambapo kutazidi kupoteza.
Hatua ya kuchukua;
Kwa maamuzi yoyote ambayo umekuwa unachukua muda kuyafanya, chukua karatasi na igawe sehemu mbili. Kwa kila chaguo la maamuzi, orodhesha faida na hasara zake, unachopata na unachopoteza.
Mwisho chagua kile ambacho kupata kuna manufaa kuliko kupoteza.
Tafakari;
Ukitaka kula lazima ukubali kuliwa pia. Kutaka kupata bila kupoteza ndiyo kimekuwa kikwazo kwa wengi kufanya maamuzi na kuchukua hatua.
Kocha.