#SheriaYaLeo (133/366); Kuwa makini na wema unaoonyeshwa.

Mara nyingi watu hukazana kuonyesha wema fulani kwa nje ili waonekane wanafanya kwa manufaa ya wengine.

Lakini ndani yao wanakuwa wameficha sababu halisi ambayo ni kujinufaisha wao wenyewe zaidi.

Kuwa makini sana na wema unaoonyeshwa kwa nguvu kubwa, kwa sababu unakuwa umeficha ulaghai mkubwa unaoendelea.

Mbinu hii hutumiwa na wengi wanaotaka madaraka au kujinufaisha ila hawataki kuonekana wazi.
Hutaka kwa nje waonekane ni wema na walioweka maslahi ya wengine mbele, kumbe ndani ni tofauti.

Sheria ya leo; Watu wanapenda kuamini kile wanachoambiwa na kuonyeshwa kwa nje. Lakini mara nyingi hayo huwa ni maigizo yanayoficha nia halisi, ambayo siyo nzuri. Unapoona mtu anatumia nguvu sana kuonekana mwema, kuwa na wasiwasi.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji