#SheriaYaLeo (135/366); Wajue viongozi wanaopenda kutukuzwa.

Katika safari yako ya maisha na mafanikio utapita maeneo mbalimbali.
Kwenye baadhi ya maeneo utakutana na viongozi ambao wanapendwa kutukuzwa.

Viongozi hao huamini hawawezi kukosea. Huona kila wanachofikiri wao ndiyo sahihi zaidi na wengine wote wanakubaliana nao.

Kufikiri tofauti na wao wanachukulia kama usaliti na kuona kama unataka kuchukua nafasi yao.

Pamoja na kupenda kwao sifa, ndani yao viongozi hao huwa hawajiamini. Hivyo hutaka watu zaidi wawasifie ili wajione wako sahihi.

Hawa ni viongozi ambao unapaswa kuwajua mapema na kuwaepuka, kwa sababu hawana jema. Haijalishi mmekuwa mnakubaliana kiasi gani, siku utakayopishana na kiongozi wa aina hiyo ndiyo siku unageuka kuwa adui na msaliti.

Sheria ya leo; Viongozi wanaopenda kutukuzwa wanaopenda kuzungukwa na watu wanaosifu tu na siyo kukosoa. Watambue viongozi hao na kujiepusha nao, usikubali kukaa chini yao kama unataka kufikiri kwa akili zako. Maana siku utakayopishana nao, ndiyo siku watakayochukua hatua zinazoweza kukuharibia sana mambo yako.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji