#SheriaYaLeo (137/366); Tambua Wanaojificha nyuma ya jadi.

Wapo watu ambao wanataka kuleta mabadiliko ya aina fulani.
Lakini wanajua jamii huwa haipo tayari kwa mabadiliko makubwa na ya haraka.

Hivyo hujificha nyuma ya jadi, kwa kujionyesha kwamba ni watu ambao wanadumisha jadi.
Wanatumia nguvu nyingi kuonekana wanakubali mfumo uliopo na wanaulinda ili uendelee kuwepo.

Lengo lao ni kupata nafasi ya kuaminiwa na kisha kuleta mabadiliko makubwa ya ndani.
Huleta mabadiliko hayo wakati ambao hakuna anayetegemea.
Mabadiliko hutokea kidogo kidogo kiasi cha watu kutokujua kama kuna mabadiliko yanayoendelea.

Watu huwa hawapendi mabadiliko, kuonyesha unataka mabadiliko ni kujizuia kupata nafasi nzuri.
Kama unataka kupata fursa nzuri ya kuleta mabadiliko, anza kwa kuonyesha unakubaliana na mfumo uliopo.

Pia kuwa makini na wale wanaojionyesha kwa nje wanadumisha jadi, ni sehemu waliyojificha ili kuweza kuleta mabadiliko wanayotaka.

Sheria ya leo; Usikubali kudanganyika na chochote ambacho watu wanaonyesha kwa nje. Tambua ndani yao wanaweza kuwa na nia tofauti kabisa.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji