#SheriaYaLeo (139/366); Angalia nyuma ya barakoa.
Kunbuka kwa kawaida watu huwa wanatengeneza mwonekano fulani wanaotaka dunia ione.
Hivyo kila mtu ni kama amevaa barakoa, akionyesha kile ambacho anataka wengine waone na kuficha nia kuu aliyonayo.
Mtu anaweza kuwa na uso wa tabasamu na maneno mazuri kabisa. Hii ni barakoa inayowafanya wengine wamwamini ni mtu mwema.
Lakini nyuma ya barakoa hiyo anakuwa ameficha ukweli wake halisi.
Kwa bahati nzuri au mbaya, sisi binadamu hatuwezi kuficha nia za kweli tulizonazo.
Lazima tu kuna kitu huwa kinatusaliti.
Mtu anaweza kuwa na uso wa tabasamu, lakini macho yake yanaonyesha hasira au ukatili alionao.
Mtu anaweza kusema mambo mazuri, lakini sauti yake na kasi yake ya uzungumzaji ikaonyesha jinsi ambavyo hana nia nzuri.
Wajibu wako ni kuweka umakini mkubwa kwa watu, kuangalia viashiria vinavyodhihirisha uhalisia wao na siyo kuhadaika na barakoa walizovaa.
Hakuna anayeweza kuficha hisia zake halisi kwa muda mrefu.
Wengi hushindwa kuzijua kwa sababu wamekosa umakini katika kuwachunguza watu.
Wanaamini kile ambacho watu wanaonyesha na hawana udadisi wowote.
Wewe usiwe hivyo, jua kuna wengi wana nia ambazo hawazionyeshi wazi na wanakutega unase kwenye mitego yao.
Kuwa na udadisi mkubwa, jua kila mtu amevaa barakoa hivyo angalia nyuma ya barakoa hiyo kujua nia halisi ya mtu.
Sheria ya leo; Jifunze kutokuhadaika na kile ambacho watu wanakuonyesha, badala yake jua nia yao halisi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji