#SheriaYaLeo (140/366); Kutaka usawa kwa kila mtu.
Njia nyingine ambayo hutumiwa sana na wale wanaotaka mamlaka bila ya kuonekana wazi wazi ni kutaka usawa kwa kila mtu.
Hapa husisitiza kila mtu ni sawa na lazima watu wote wachukuliwe kwa usawa.
Hukazana kuwaaminisha wengine kwamba uwezo, uimara na hadhi tofauti za watu havina maana yoyote.
Watu hao kwa nje huonekana wanatetea usawa, lakini kwa ndani wana nia ya tofauti.
Kwa kuwachukulia watu wote kwa usawa, wanajipa mamlaka ya kutoa manufaa kwa watu kwa vile wanavyotaka wao, kitu wanachotumia kuwadhibiti wengine.
Ukweli ni kwamba watu hatupo sawa, tunatofautiana sana kwenye uwezo, vipaji, uimara, madhaifu na hata hadhi.
Tunafanya vitu vinavyotofautiana kabisa.
Na kutokana na tofauti hizo, baadhi ya watu wanakuwa na umuhimu mkubwa kuliko wengine.
Hiyo ni kanuni ya asili ambayo huwezi kupingana nayo.
Kuwachukulia watu wote kwa usawa unaishia kutengeneza tatizo jingine kubwa zaidi.
Kwani utajikuta unawapandisha wasio na uwezo na kuwadidimiza wale wenye uwezo mkubwa.
Unaweza kufikia huo usawa kwa nje, lakini ukawa umepoteza vitu vingi vikubwa na vya kipekee.
Watu hawalingani na hivyo usawa kamili kwa wote ni kitu ambacho hakiwezi kuwepo.
Unapomuona mtu anayekazana kuwepo kwa usawa kwa wote, jua anataka kupata mamlaka ya kuwatawala wote.
Sheria ya leo; Wale wanaotaka watu wote wachukuliwe sawa wanatumia njia hiyo kuficha nia yao kuu ambayo ni kupata mamlaka ya kuwadhibiti watu wote. Wachukulie watu kulingana na ukubwa, ubora na thamani ya kile wanachofanya.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji