#SheriaYaLeo (143/366); Tambua uimara wa tabia za watu.

Tabia za watu zina nguvu kubwa kwenye maisha yao.
Mtu mwenye tabia dhaifu, itadhoofisha hata sifa nyingine alizonazo.

Kwa mfano mtu mwenye akili sana lakini mwenye tabia dhaifu, anaweza kuja na mawazo mzuri sana na hata kufanya kazi bora.
Lakini wanapokutana na msongo wanashindwa kuhimili, au hawawezi kukabiliana na ukosoaji wa wengine.
Kwa vyovyote vile kuna namna udhaifu wao wa tabia utakuwa kikwazo kwao licha ya mazuri wanayokuwa wamefanya.

Ni muhimu sana kujua uimara wa tabia za watu kabla hujaamua kushirikiana nao.
Kwa sababu tabia za wale unaoshirikiana nao zitakuathiri pia.

Mtu mwenye tabia imara, hata kama hana akili sana unaweza kumtegemea zaidi kuliko mwenye akili sana na tabia dhaifu.
Watu wenye tabia imara ni wachache na adimu sana.
Unapokutana nao, hakikisha hupotezi fursa ya kushirikiana nao, maana ni hazina kubwa.

Sheria ya leo; Katika kupima uimara au udhaifu wa tabia za watu, angalia historia zao za nyuma namna wamekuwa wakikabiliana na magumu na kuchukua uwajibikaji. Angalia mwendelezo wao, ni vitu gani hasa walivyoweza kumaliza au kukamilisha?

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji