#SheriaYaLeo (146/366); Waepuke wapenda drama.
Kuna watu ambao wanatumia drama kama njia ya kuwatawala watu wengine.
Watu hawa ni wazuri sana kwenye kutengeneza mambo na kuigiza kwa namna ambayo wataonekana wanaonewa.
Wanahakikisha wanawateka wengine kihisia ili wayaamini maigizo yao, wakitafuta zaidi huruma.
Watu hawa wana hadithi na mapito mengi ambapo kila wakati wao ndiyo wanaoonewa, kuumizwa na kudhulumiwa.
Katika hadithi zao hizo wao ni wema mara zote na wengine ndiyo wabaya.
Huwa wanataka uwe upande wao na uwatetee katika mambo yao.
Ukishanasa kwenye mtego huo wanakutumia vile wanavyotaka wao.
Na ili kuhakikisha hujinasui, wanakufanya uwe sehemu ya drama.
Kila unapotaka kujinasua wanakufanya ujione una hatia kama utawaacha.
Hawa ni watu ambao wamejifunza hivyo tangu utotoni.
Wamepitia mazingira ambayo hakukuwa na waliowajali na kuwapenda.
Hivyo walijifunza kutengeneza drama ili kuwateka wengine wawajali.
Watu hawa huwa hawana kingine chochote kinachoweza kuwafanya watu wawajali na kuwafuatilia zaidi ya drama zao.
Na ndiyo maana huzitumia sana na kuendelea kuzikuza.
Sheria ya leo; Ni vyema uwajue wapenda drama mapema kabla hujanasa kwenye mtego wao. Angalia mapito yao kupata ushahidi wa yale wanayotengeneza. Ukishajua mtu ni mpenda drama kimbia haraka kwani ukishanasa kwao ni vigumu kujinasua.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji