#SheriaYaLeo (147/366); Mtego wa uaminifu.
Uaminifu wa kweli ni sifa ambayo inapatikana kwa watu wachache sana.
Na pia ndiyo sifa inayotumika sana na wale wenye hila ya kujinufaisha kupitia wengine.
Wanaigiza kama ni watu waaminifu sana ili wale wanaowalenga wawaamini.
Na hapo wakishawaamini basi wanapata kile wanachotaka.
Mfano mtu anaweza kuwa anataka kupata taarifa fulani za siri kutoka kwa mwingine.
Hivyo anaanza kwa kujifanya anamweleza siri zake, mtu huyo anayeelezwa siri anashawishika na yeye kutoa siri zake.
Kumbe siri ambazo mtu alitoa siyo kweli, ilikuwa tu ni njia ya kumtega.
Sisi binadamu ni wadhaifu sana kwenye uaminifu.
Tunapoona mtu ni mwaminifu basi tunamwamini moja kwa moja bila ya shaka yoyote.
Wengi wenye nia zao binafsi huwa wanatumia sana mtego huu wa uaminifu wa kuigiza.
Ni wajibu wako kutokushawishika na uaminifu unaoonyeshwa kwa nje.
Mchunguze mtu kwa ndani na ukweli utaujua, nia yake halisi itakuwa hadharani.
Na kiashiria cha kwanza kujua kama mtu siyo mwaminifu kweli ni pale unapotaka athibitishe vitu fulani.
Atajifanya kukuuliza kwa ukwali kwamba ina maana humuamini?
Anapokuwa kwenye dalili zozote za aina hiyo, za kutaka umwamini tu bila kuthibitisha, jua ni mtego amekuwekea unase.
Sheria ya leo; Kwa kuigiza kama wameutoa moyo wako kwako, wale wenye nia fulani wanajua utanasa kwenye mtego na kuutoa moyo wako kwao. Wanajifanya kukiri vitu fulani kwako ambao ni uongo, ili kukutega wewe ukiri ukweli utakaowanufaisha.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji