#SheriaYaLeo (148/366); Jua nia zao halisi.
Kwa kawaida sisi binadamu ni wabinafsi.
Huwa hatufanyi mambo kama hayana manufaa kwetu.
Hivyo kwa kila jambo ambalo watu wanafanya, jua kuna manufaa fulani wanayoyapata.
Mara nyingi hilo linaweza lisiwe wazi.
Wengi wenye nia isiyo njema huwa wanaificha.
Wanatengeneza mwonekano fulani wa kuficha nia zao za ndani.
Hilo halinaanishi kwamba nia hizo hazipo.
Ili kujua nia halisi ya kila linalofanyika, anza kwa kujiuliza ni nani anayenufaika.
Kwa jambo lolote linalotokea, jiulize lina manufaa gani na kwa watu gani.
Kwa kuanzia hapo utaweza kujua nia halisi ya wale wanaofanya au walio nyuma ya jambo hili.
Usiamini na kuchukulia mambo kwa namna yanavyoonekana nje tu.
Jua kwa ndani mambo yanaweza kuwa tofauti kabisa.
Sheria ya leo; Usidanganyike na mwonekano wa nje. Kwa kila kinachotokea na kwa kila ambacho watu wanafanya na kusema, jiulize ni kwa manufaa gani? Nani ananufaika na ananufaikaje? Mara zote kumbuka dunia inaendeshwa kwa maslahi binafsi ya watu.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji