#SheriaYaLeo (151/366); Kila mtu anataka mamlaka zaidi.

Watu huwa wanafanya yale wanayofanya ili kupata mamlaka zaidi.

Ipo kauli kwamba mamlaka huwa yanawaharibu watu.
Lakini kinyume chake pia ni kweli.
Kukosa mamlaka kunawaharibu watu pia.

Hakuna anayeweza kuvumilia hali ya kutokuwa na mamlaka.
Hivyo mtu hufanya lolote ili tu kupata mamlaka.

Kuna mambo watu wanaweza kufanya na ukashindwa kuelewa kabisa.
Ila unapogundua kwamba kila mtu anataka mamlaka zaidi, unaelewa kwa nini watu wanafanya yale wanayofanya.

Kudanganya, kuhadaa, kuiba, kulaghai, kujipendekeza na hata kuwasaliti wengine, yote hayo yanasukumwa na hitaji la watu kutaka mamlaka zaidi.

Sheria ya leo; Unapokuwa na wasiwasi au huelewi kwa nini watu wanafanya au kusema vitu fulani, tambua kwamba kila mtu anataka mamlaka zaidi. Hivyo chochote wanachofanya ni kuhakikisha wanayapata mamlaka hayo.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji