#SheriaYaLeo (152/366); Mjue vizuri unayekabiliana naye.

Uwezo wa kuwajua vizuri watu kwa undani ni hitaji muhimu sana kwenye kupata na kutunza mamlaka.
Bila ya uwezo huo unakuwa kipofu anayefanya mambo kwa kubahatisha.
Kwa sababu utachagua kukabiliana na watu wasio sahihi au wakiwa sahihi utashindwa kuwajua vizuri.

Kabla ya kukabiliana au kushirikiana na yeyote, hakikisha umemjua kwa undani.
Bila ya kufanya hivyo utaishia kupoteza muda na nguvu zako bure.

Wajue watu nje ndani, jua uimara wao na madhaifu yao. Jua nini wanahofia na yale wanayojigamba nayo.

Kuna mambo mawili muhimu ya kuzingatia katika kuwajua unaokabiliana nao.

Moja ni usiamini hisia zako.
Hisia zinaweza kukudanganya na ukaondoka na yasiyo sahihi.
Kusanya taarifa za kutosha kuhusu watu ili kuweza kujua kwa undani.

Mbili ni usiamini kile watu wanakuonyesha kwa nje.
Watu huwa ni wazuri sana kuigiza ili kukuhadaa.
Kile wanachoonyesha kwa nje ni tofauti kabisa na kilicho ndani.
Jua undani wa watu na siyo kuchukua walivyo nje.

Sheria ya leo; Hakuna manufaa yoyote utakayoyapata kwa kutokuwajua watu kwa undani. Jifunze kujua tofauti kati ya simba na kondoo, la sivyo utalipa gharama kubwa.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji