#SheriaYaLeo (156/366); Tumia udhaifu wa watu kuamini mwonekano wa nje.

Ni asili yetu binadamu kuamini kwa haraka kile ambacho tunakiona.
Huwa hatuna muda wa kuchunguza kwa undani na kujua nia halisi ya mtu.

Hivyo unaweza kutumia udhaifu huu kukubalika na wengine na kupata kile unachotaka.

Unachopaswa kufanya ni kutengeneza mwonekano wa nje ambao una ushawishi kwa wengine.
Mwonekano ambao unawafanya waamini kile wanachotaka kuamini na kisha kukupa kile unachotaka kupata kutoka kwao.

Japo njia hii inaweza kutumika kwa ubaya, kuwahadaa watu waamini kitu kisichokuwa halisi, bado unaweza kuitumia kwa uzuri.
Unaweza kutumia njia hii kuwasaidia watu waweze kuamini kile chenye manufaa kwao.
Maana wakati mwingine watu wanaweza kupinga hata kitu ambacho kina manufaa kwao.

Jua watu wanataka kuona nini na kisha tengeneza mwonekano wa nje unaowafanya waone kitu hicho na kuamini kisha kuchukua hatua unayotaka wachukue.

Sheria ya leo; Tengeneza mwonekano wa nje wenye ushawishi kwa wale unaowalenga. Kwa sababu watu wanaamini sana mwonekano wa nje.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji