#SheriaYaLeo (157/366); Waweke watu kwenye shauku ya kukufuatilia.

Watu huwa wanapenda kufuatilia vitu ambavyo vinawaweka juu juu.
Vitu ambavyo hawana uhakika vitakwendaje.
Vitu ambavyo ni tofauti kabisa na mazoea na hivyo havitabiriki.

Kwa kila unachofanya, kifanye kwa namna hiyo na siyo kwa mazoea.
Wafanye watu wawe wanajiuliza kipi kingine utafanya maana hawana uhakika wa nini unakwenda kufanya.

Ukifanya kwa mazoea watu wanakuwa hawana shauku ya kukufuatilia, kwa sababu wanajua hakuna jipya.
Ila ukifanya kwa utofauti kila wakati, watu wanakuwa na shauku kubwa ya kukufuatilia maana hawajui nini kinakwenda kutokea.

Tumia utofauti kuteka umakini wa watu ili wakufuatilie kwa karibu kwa kila unachofanya.
Kwa njia hiyo utaweza kujenga ushawishi mkubwa kwa watu hao.

Sheria ya leo; Tumia utofauti kuwashangaza na kuwahamisha watu. Jifunze kuyapanga matukio yako kwa namna ambayo kila mtu anasubiria kwa shauku kubwa nini kitatokea. Usifanye kwa mazoea na wala usiweke mbinu zako zote wazi. Nenda hatua kwa hatua ili kuwateka watu wazidi kukufuatilia.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji