#SheriaYaLeo (163/366); Mwondoe mwenye ushawishi.

Kwenye kundi lolote lile huwa kuna mtu mmoja mwenye ushawishi mkubwa na ambaye wengine wote wanamsikiliza.

Na hata kunapokuwa na matatizo, chanzo chake kikuu huwa ni mtu mmoja mwenye ushawishi.
Pale anapokuwa hajaridhika kwa namna fulani anakuwa tayari kusambaza hilo kwa wengine na kuwa chanzo cha matatizo.

Ili kuleta utulivu na kupata udhibiti wa kundi lolote lile, unapaswa kumtambua na kumwondoa yule mwenye ushawishi kwa wengine.

Huyo huwa ndiyo chanzo cha mambo yote yanayoendelea kwenye kundi hilo.
Bila ya kumwondoa, mambo yatazidi kuwa mabaya.

Unapompiga mchungaji, kondoo wote hutawanyika kwa sababu wanakosa kiongozi wa kumfuata.
Hivyo ndivyo unavyopaswa kufanya pale kunapokuwa na changamoto kwenye kundi lolote lile, kumwondoa yule mwenye ushawishi zaidi kwa wengine.

Kutokana na ushawishi wao ambao pia ni sumu, njia pekee ni kuwaondoa kabisa watu hao.
Usijidanganye kwamba unaweza kuwadhibiti wakiwa ndani ya hilo kundi.
Watazidi kutengeneza matatizo zaidi kwa ushawishi wao.
Kuwaondoa mara moja ndiyo njia ya uhakika ya kumaliza matatizo yaliyopo.

Sheria ya leo; Pale kiongozi anapoondoka, mhimili mzima unaanguka kwa sababu hakuna kinachokuwa kimewashikilia watu. Kwa kumwondoa mtu mwenye ushawishi, unakuwa umeyamaliza matatizo aliyokuwa anayasababisha.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji