#SheriaYaLeo (164/366); Tumia mbinu ya kujisalimisha.
Unapokuwa dhaifu, usipambane na mwenye nguvu.
Badala yake chagua kujisalimisha.
Kupambana na mwenye nguvu huku wewe ukiwa dhaifu ni kuchagua kushindwa vibaya.
Kujisalimisha kunakupa nafasi ya kujipanga na kukusanya nguvu zako ili baadaye uweze kushambulia na kushinda.
Kujisalimisha kunamfanya adui yako akudharau na kukuona huna madhara.
Hilo linakupa nafasi ya kuimarisha nguvu zako wakati nguvu za adui zikizidi kupungua.
Watu wanaotaka kuonekana wana mamlaka huwa wanafanganyika kirahisi na mbinu hii ya kujisalimisha.
Unapojisalimisha wanakudharau na hilo linakupa nafasi ya kuweza kujibu mashambulizi na kuwaathiri vibaya.
Hakuna ufahari kupambana pale unapogundua huna nguvu za kutosha, ni kujipeleka kwenye anguko.
Jisalimishe, utadharaulika lakini hilo litakupa nafasi ya kujijenga vizuri na kuja kushambulia kwa nguvu kubwa na kupata ushindi mkubwa.
Sheria ya leo; Unapojikuta huna nguvu za kupambana, kujisalimisha ndiyo mbinu pekee ya kukupa nafasi ya kujipanga vizuri kwa ajili ya baadaye. Kujisalimisha kunaficha nia yako halisi, kunakufundisha uvumilivu na kukidhibiti, vitu vinavyohitajika sana ili kupata ushindi baadaye.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji