#SheriaYaLeo (169/366); Tumia mwonekano kushawishi.
Watu huwa wanashawishika sana na mwonekano wa vitu ulivyo.
Vitu kama rangi, muundo na mpangilio wa vitu vina nguvu ya kuwashawishi watu kwa namna fulani.
Kwa mfano matumizi ya rangi nyekundu kwenye maandishi yanawafanya watu waone kitu ni muhimu na cha haraka hivyo kushawishika kuchukua hatua haraka.
Watu hawana muda wa kuchunguza kila kitu, hivyo wanatumia njia ya mkato ya kuangalia mwonekano wa nje kufanya maamuzi.
Hata kama una kitu kizuri na sahihi kabisa, usipokitengenezea mwonekano wenye ushawishi, hakitaweza kuwafikia wale unaowalenga.
Sheria ya leo; Kamwe usidharau jinsi unavyopangilia vitu. Jinsi vitu vinavyoonekana kama kwa rangi ina ushawishi mkubwa kwa watu. Tumia mwonekano huo kuwa na ushawishi zaidi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji