#SheriaYaLeo (172/366); Onyesha udhaifu wako.
Jifunze kugeuza udhaifu wako kuwa njia ya kupata mamlaka.
Pale unapoonekana imara na mkamilifu wakati wote, watu wanaweza kuona wewe siyo wa aina yao.
Katika nyakati fulani unapaswa kuwaonyesha watu udhaifu wako ili waweze kuona wewe ni kama wao, na kukuamini zaidi. Hila linakufanya uwe na ushawishi zaidi kwao.
Lakini epuka sana kutumia udhaifu wako kama njia ya kutengeneza huruma kwa wengine.
Usionyeshe udhaifu wako kila mara na kwa kila mtu.
Badala yake uonyeshe mara chache na kwa wale ambao tayari mmeshajuana kwa undani.
Japokuwa mara nyingi unapanga kuonekana imara na mkamilifu.
Mara chache na kwa wachache onyesha udhaifu wako, hilo litakusaidia kuaminika zaidi.
Sheria ya leo; Usikazane sana kuficha udhaifu wako mara zote. Badala yake utumie udhaifu huo kujenga imani zaidi kwa watu, kwa kuuonyesha kwao. Hilo litawafanya wakuone wewe ni kama wao walivyo na madhaifu mbalimbali.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji