#SheriaYaLeo (173/366); Chukua mamlaka tararibu.
Ukionekana una haraka sana ya kuchukua mamlaka, utaishia kuibua hasira, wivu na chuki.
Watu hawatakuwa tayari kukuachia uchukue mamlaka kwa vile unavyotaka.
Hivyo njia bora ni kuchukua mamlaka hayo taratibu.
Kujipa muda wa kutosha katika kukamilisha hilo.
Kwanza wape watu nafasi ya kuona wanafanya kwa mamlaka yao wenyewe.
Kisha wape mapendekezo ya kuboresha zaidi kile wanachofanya.
Ni kupitia mapendekezo hayo ndiyo unachukua mamlaka zaidi na watu hao kujikuta wanafanya vile unavyotaka wewe.
Ukianza kwa kuwaambia wafanye unavyotaka wewe, hilo halitafanikiwa.
Kwani hata kama inabidi wakusikilize, watafanya vibaya kwa makusudi ili tu kukuangusha.
Lakini unapoanza kwa kuwapa uhuru wa kufanya kwa namna wanavyotaka wao, wanajitoa kufanya kwa ubora zaidi.
Na unapowapa mapendekezo ya kuboresha, wanayachukua na kufanyia kazi.
Unaenda hivyo kidogo kidogo mpaka unakuwa na mamlaka kamili ya kile wanachofanya.
Sheria ya leo; Kuchukua mamlaka kwa wazi na kwa haraka ni jambo la hatari kwani inaibua hasira, wivu, chuki na kutokuaminika. Njia bora ni kuchukua mamlaka taratibu, kujipa muda wa kutosha katika hilo.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji