#SheriaYaLeo (177/366); Tengeneza hali ya usiri.

Watu wanapoelewa na kuzoea mtu au kitu huwa wanakidharau.
Hiyo ni kwa sababu hakuna chochote kinachokuwa kinawasukuma kufuatilia ili kujua zaidi.

Kama unataka watu wakufuatilie, tengeneza hali ya usiri.
Fanya mambo ambayo watu hawayaelewi au hawawezi kuyaelezea.
Kuwa na mwonekano wa tofauti ambao watu hawajauzoea.

Hayo yatawafanya watu wakufuatilie kwa karibu zaidi ili kujua maana ya yale unayofanya.
Pale watu wanapokufuatilia ndiyo unaweza kutumia fursa hiyo kukamilisha yale unayotaka kupitia watu hao.

Inaweza kuwa ni kuwashawishi wakubaliane na wewe kwenye kitu fulani.
Au kuwashawishi wanunue kitu unachouza.
Au kingine chochote unachotaka kupitia watu hao.

Anza kwa kutengeneza hali ya usiri, hiyo itawavuta wengi kwako na kukupa fursa ya kuwashawishi wakupe kile unachotaka.

Sheria ya leo; Watu wanapenda kufuatilia vitu wasivyovielewa na vyenye siri kubwa. Watengenezee hali hiyo na utawavuta kwako kisha kuweza kupata kile unachotaka kutoka kwao.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji