#SheriaYaLeo (179/366); Waambie watu wanachotaka kusikia.

Ukweli huwa unauma,
Watu wengi huwa hawapendi kusikia ukweli.
Hivyo kama unataka kupata wafuasi wengi, usiwaambie watu ukweli, bali waambie kile wanachotaka kusikia.

Watu hawataki kusikia kwamba kujenga utajiri kunahitaji muda, juhudi na nidhamu ya hali ya juu.
Wanataka kusikia wakipanda pesa leo kesho wanavuna mara kumi.
Na ndiyo maana utapeli kwenye fedha hauishi.

Watu hawataki kusikia kwamba kupunguza uzito wanahitaji nidhamu kubwa kwenye ulaji na kufanya mazoezi.
Wanataka kusikia ukinywa kidonge unapunguza uzito wote wa ziada.

Kama unachotaka ni idadi kubwa ya watu wakufuate na kukukubali basi waambie kile wanachotaka kusikia, watakuona wewe ni chanzo cha raha kwao.

Kama unachotaka ni kupata watu sahihi, waambie ukweli kama ulivyo, lakini jua utawapata wachache sana.

Sheria ya leo; Maisha ni magumu na watu wamevurugwa. Hawataki tena kusikia ukweli ambao unawaumiza. Wanataka kusikia habari njema za urahisi wa kupata wanachotaka. Unapokuwa chanzo cha kuwaambia watu kile wanachotaka kusikia, watakuja kwako kwa wingi.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji