#SheriaYaLeo (189/366); Onekana kuwa kitu kinachopendwa.

Watu huwa wanapenda kitu ambacho tayari kinapendwa na watu wengine.
Kile ambacho tayari ni maarufu huwa kinawavutia watu wengine wengi zaidi.

Watu huwaepuka watu ambao watu wengine wanawaepuka na kuvutiwa na watu ambao watu wengine wanavutiwa nao.

Ili kujenga ushawishi na kuwavuta watu wengi kuja kwako, tengeneza hali ya kuhitajika na wengi.
Wafanye watu wavutiwe kuja kwako na kutaka kujihusisha na wewe.

Wafanye watu washindane kukupata na iwe ifahari kwao kama watakupata na kuwa na wewe.

Hilo litawezekana kwa kujenga hali ya umaarufu kwa kuonekana ukiwa na watu mbalimbali ambao tayari ni maarufu.

Watu wanapenda na kuvutiwa na kile kinachopendwa na wengi.
Tengeneza hali hiyo ili uweze kuwavutia wengi kuja kwako na kuwa na ushawishi mkubwa kwao.

Sheria ya leo; Jenga sifa ambayo imekuzidi wewe, sifa ya kukubalika na kuhitajika na wengi. Pale wengi wanapovutiwa kwako, hilo linawafanya wengi zaidi kuvutiwa kuja kwako.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji