2687; Ya kwangu ni tofauti.

Kushauri wengine ni rahisi, lakini wewe mwenyewe kutumia ushauri huo huo unaowapa wengine ni ngumu, kwa sababu unaona hali yako ni tofauti.

Kuwakosoa na kuwahukumu wengine pale wanapokosea ni rahisi.
Lakini pale wewe unapofanya makosa hayo hayo unajitetea kwamba hali yako ni tofauti. Hujihukumu na kujikosoa kama unavyofanya kwa wengine.

Unapoona wengine wanapiga hatua unaona ni rahisi kwao.
Unapotakiwa na wewe upambane kama wao ili upige hatua unaona hali yako ni tofauti hivyo hutaweza kupiga hatua kama zao.

Rafiki, leo napenda nikukumbushe kwamba unajidanganya.
Hali yako siyo tofauti sana kama unavyoichukulia.
Hutofautiani sana na wengine.
Kitu pekee kinachokufanya uone ni tofauti ni fikra zako mwenyewe.

Lakini pale unapokubali kile unachokiona kwa wengine na kukifanyia kazi, lazima utapata matokeo mazuri.

Hatua ya kuchukua;
Jikumbushe ni mambo gani unajua unapaswa kufanya ili ufanikiwe, lakini umekuwa unajiambia hayafai kwako au hali yako ni tofauti.
Sasa ndiyo wakati wa kufanya yote unayopaswa kufanya ili uweze kupata unachopaswa kupata.

Tafakari;
Kikwazo kikuu cha mafanikio ni kujidanganya mwenyewe. Na hakuna mtu rahisi kwako kumdanganya kama wewe mwenyewe.
Kuwa na tahadhari kubwa kwenye mambo mengi unayojiambia, mengi ni uongo wa kuepuka kukabiliana na mambo magumu.

#Let’sBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining