#SheriaYaLeo (194/366); Vuruga Matarajio Yao.
Mazoea ni kifo cha ushawishi.
Kama watu wanajua kila kitu kuhusu wewe, wameshazoea na kutegemea vitu fulani kutoka kwako, hawawezi kuvutiwa kushawishika na wewe.
Wanaona mambo ni yale yale na hakuna cha tofauti.
Ili kuendelea kuwa na ushawishi unahitaji kuvuruga matarajio ambayo watu wanayo kwako.
Unapaswa kwenda kinyume na mazoea yako na kufanya vitu ambavyo hujazoea kufanya.
Hilo linawafanya watu wasiweze kukutabiri na wasijue ni nini utafanya kwenye hali fulani.
Kwa kuwaweka kwenye hali hiyo, watakuwa na hofu na mashaka wasijue nini kitakachoendelea.
Ni hali hiyo ya hofu na mashaka pamoja na kukosa uhakika ndiyo itawafanya wakufuatilie zaidi na hapo kushawishika zaidi na wewe.
Jenga hali ya usiri kuhusu mambo yako na hilo litafanya uwe na ushawishi zaidi kwa wengine.
Sheria ya leo; Usiweke kila kitu chako wazi, vuruga matarajio ambayo watu wanayo kwako na pia potea ili kuwaweka watu kwenye hali ya hofu na wasiwasi kitu kitakachoongeza ushawishi wako kwa wengine.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji