#SheriaYaLeo (197/366); Chochea ushawishi wako.
Kuna wakati inatokea mtu unayetaka kumshawishi anaonekana kuwa wa viwango vya juu zaidi kuliko wewe.
Anakuwa mtu ambaye hana anachoshawishika nacho kwako.
Hapa ndipo unahitaji kuwa na mbinu za ziada za ushawishi kwa watu wa aina hiyo.
Unachohitaji ni kutengeneza ukaribu ambao unaongeza ushawishi kwa watu hao.
Pia hali kama kuwapa watu zawadi na kwenda nao kwenye matukio yanayowafanya wajisikie vizuri inaongeza zaidi ushawishi wako kwao.
Haijalishi hata kama mtu ni wa viwango vya juu kuliko wewe, bado unaweza kuwa na ushawishi kwake kama utatumia fursa sahihi kufanya hilo.
Sheria ya leo; Aina yoyote ya hisia kali ambazo unaweza kutengeneza kwa mtu huwa zinachochea sana ushawishi. Hisia za watu zinapokuwa juu, wanashawishika kwa urahisi zaidi bila kujali tofauti mlizonazo.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji