#SheriaYaLeo (200/366); Jithibitishe Kwao.
Kujithibitisha kwa wengine ni kwa namna gani umejitoa kwa ajili yao kunaongeza sana ushawishi.
Kunajenga hisia kali kwao na kuficha nia ya ndani unayoweza kuwa nayo.
Kafara unazojitoa na mambo unayopoteza vinapaswa kuwa wazi kwao waone.
Kuongelea tu au kueleza ni kiasi gani vimekugharimu itaonekana kama kujisifia.
Kosa usingizi, umwa, poteza muda wako, weka kazi yako kwenye hatari, tumia fedha nyingi kuliko unavyoweza kumudu. Zote hizo ni njia za kuonyesha kwao ni jinsi gani umejitoa.
Unaweza kuonyesha yote hayo kwa namna ya kupitiliza, lakini kamwe usionekane kujisifia au kuonyesha unajutia.
Jiweke kwenye maumivu na waache wajionee wenyewe.
Kwa kuwa karibu kila mtu anaonekana kuwa na nia fulani kwenye kile anachofanya, wewe utaonekana umejitoa kweli na ushawishi wako utakuwa mkubwa.
Sheria ya leo; Chagua matukio magumu na yanayoonekana yatakayoonyesha jinsi ulivyojitoa kweli kwa ajili ya watu. Hilo litaongeza sana ushawishi wako kwao.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji