2698; Majuto hayana nafasi.

Kuna fursa ulishindwa kuitumia kipindi cha nyuma na hivyo kushindwa kunufaika nayo.

Badala ya kupoteza muda wako kwenye kujutia hilo, unapaswa kulitumia kama funzo la kutokubali kukosa fursa nyingine nzuri.

Kuna makosa uliyafanya huko nyuma ambayo yalikugharimu sana.

Badala ya kupoteza muda kwenye kujutia makosa hayo, yatumie kama funzo la kutokuyarudia tena.

Kwenye kitabu cha THINK AND GROW RICH mwandishi anashirikisha kisa cha bwana mmoja aliyeona fursa kwenye uchimbaji wa dhahabu.
Akanunua vifaa na kwenda kuchimba.
Mwazo alipata dhahabu kwa kiasi, lakini baadaye zikaisha.
Akaendelea kuchimba lakini akawa hapati dhahanu.
Akachimba tena na tena lakini hakupata kitu.
Baadaye akaamua kuuza migodi na mashine zake kwa hasara na kwenda kwenye biashara nyingine.

Yule aliyenunua migodi na mashine hizo aliitafiti miamba kwa kina na akachimba kidogo tu, akaweza kukutana na dhahabu nyingi sana.
Unafikiri aliyeuza migodi ile alijisikiaje baada ya kupata taarifa hizo?
Hapo ndipo penye somo kubwa, alijiambia; nimekata tamaa nikiwa nimebakiza sehemu ndogo kupata dhahabu nyingi, sitakuja kukatishwa tamaa na kitu chochote.
Na kweli kwenye biashara yake mpya alipata mafanikio makubwa sana.

Haijalishi umefanya au kutokufanya nini, usikubali kuwa na majuto.
Jifunze kwa yale unayopitia na fanya kwa ubora zaidi.

Majuto hayana faida yoyote, ni kile unachojifunza na kufanyia kazi ndiyo chenye manufaa.

Hatua ya kuchukua;
Ni mambo gani unayajutia kwenye maisha yako?
Kuanzia sasa ondokana na majuto, jifunze na kuwa bora, lakini siyo kujutia.

Tafakari;
Kila jambo unalopitia lina sababu.
Na kila unalopitia kuna namna unaweza kulitumia kwa ubora zaidi.
Usisumbuke na majuto, angalia kipi bora zaidi unachoweza kufanya.

#Let’sBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining