#SheriaYaLeo (202/366); Kuwa chanzo cha raha.
Hakuna mtu anayependa kusikia kuhusu matatizo yako.
Sikiliza matatizo na malalamiko ya wale unaowalenga, lakini muhimu zaidi waondoe kwenye matatizo hayo kwa kuwapa raha.
Kadiri unavyokuwa chanzo cha raha, ndivyo wengi wanavyovutiwa na kushawishika na wewe.
Mwonekano wa nguvu na ucheshi una ushawishi kuliko mwonekano wa uchovu na ukali.
Kwa kuwa watu huwa wanapenda kujihusisha na vile vinavyowapa raha, kuwa chanzo cha raha kunaongeza ushawishi wako kwa wengine.
Sheria ya leo; Kuwa mcheshi na mwenye kusifis kuna ushawishi kuliko kuwa mchovu na mkosoaji.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji