#SheriaYaLeo (203/366); Sheria ya tamaa.
Watu huwa wanatamani kile ambacho wengine wanacho.
Haijalishi kina ubora kiasi gani, kitendo cha wengine kuwa nacho, kinawasukuma wao kutaka kuwa nacho ili wasipitwe.
Ndiyo maana vitu vikishapata umaarufu huendelea kuwa maarufu.
Kwa sababu kila mtu anavitamani vitu ambavyo ni maarufu.
Ili kuwa na ushawishi mkubwa kwa wengine, acha kujiangalia wewe mwenyewe unataka nini na anza kuangalia wengine wanataka nini.
Wape wengine kile wanachotaka na hilo litawasukuma wengi zaidi kutaka kupata kitu hicho pia.
Hilo litafanya uwe na ushawishi mkubwa kwa wengine.
Watu hawataki ukweli kama wanavyoweza kuwa wanasema.
Wanachotaka watu ni kuridhisha tamaa zao.
Wape watu hilo na watashawishika sana na wewe.
Sheria ya leo; Wahadae watu na umaarufu, kile ulichonacho au unachofanya kinapaswa kuonekana kila mahali hali itakayochochea tamaa kwa wengine wengi kutaka kuwa nacho pia. Hilo litaongeza ushawishi wako kwa wengine.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji