2700; Kama wengine wanafanya, usifanye.
Huwezi kupata mafanikio makubwa kama utaendelea kufanya vitu kwa namna ambavyo wengine pia wanavifanya.
Ni lazima ufanye vitu tofauti au kwa utofauti na wengine wanavyofanya.
Hiyo ni lazima kama unataka kupata mafanikio makubwa.
Kamwe usifanye kitu ambacho wengine pia wanakifanya au kwa namna wanavyokifanya.
Mara zote fanya vitu tofauti au kwa utofauti na wanavyofanya wengine.
Dhana ni kwamba, kama utafanya vitu tofauti au kwa utofauti na wanavyofanya wengine, kuna fursa kubwa ya kupata matokeo ambayo wengine hawayapati.
Huhitaji kutafuta siri yoyote ya mafanikio, wewe angalia tu nini wengine wanafanya, halafu wewe fanya kwa utofauti.
Wafanyabiashara wenzako wanasubiri wateja waje kwenye biashara, wewe toka uende ukawafuate wateja kule walipo.
Wenzako wanafungua biashara/kazi kwa kuchelewa na kufunga mapema, wewe fungua mapema na chelewa kufunga.
Kwa vyovyote vile, usikubali kufanya kile ambacho wengine wanafanya au kwa namna ambavyo wengine wanafanya.
Hata kama watu wote wanatembea kwa kutumia miguu, wewe tembea kwa kujiamini zaidi na kwa ukakamavu. Hilo tu linatosha kukutofautisha sana na wengine na likakupa fursa ambazo wengine hawawezi kuzipata.
Usiseme huna unachoweza kufanya tofauti au kwa utofauti.
Unayataka mafanikio, utofauti ni lazima.
Chagua wapi unakuwa tofauti na kuwa na msimamo kwenye hilo, ndipo mafanikio yalipo.
Hatua ya kuchukua;
Kwenye eneo ulilochagua kuyapata mafanikio yako, angalia jinsi gani wengine wanafanya, kisha wewe fanya kwa utofauti kabisa.
Fanya yale ambayo wengine hawayafanyi au kwa namna ambavyo wengine hawafanyi.
Tafakari;
Hakuna aliyewahi kufanikiwa kwa kufanya yale ambayo wengine wanafanya na kwa namna wanavyoyafanya.
Wewe hutakuwa wa kwanza kubadili hilo.
Hivyo badala ya kukimbizana na kuiga wengine, kuwa tofauti.
#Let’sBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining