#SheriaYaLeo (204/366); Tengeneza kidonda.

Watu huwa hawashawishiki kama hawajioni wakiwa na uhitaji.
Hivyo unachopaswa kufanya ili kuwa na ushawishi kwa watu ni kuwafanya waone wana uhitaji.

Unafanya hilo kwa kutengeneza kidonda ndani yao.
Kwa kujua madhaifu yao au kile wanachokosa na kuweka mkazo zaidi kwenye hilo.

Kwa kuwaonyesha wanaweza kuwa bora zaidi au kupata zaidi ya walichonacho, unaibua tamaa ndani yao ya kutaka zaidi.

Kwa kuona hawajakamilika au kupata kile wanachotaka, watu wanakuwa tayari kukusikiliza ili wapate zaidi.

Kila mtu ana uhitaji, udhaifu au maumivu yaliyo ndani yake.
Ukiweza kuyagusa hayo lazima utakuwa na ushawishi mkubwa kwa wengine.

Sheria ya leo; Jiweke kama mtu unayekuja kwa wengine na mabadiliko, ukiwasaidia kuvuka yale ambayo ni kikwazo kwao na kuwawezesha kufanya makubwa zaidi. Wafanye waone pale walipo siyo sahihi au hapawatoshi na hilo litaibua tamaa ya kutaka zaidi kitu kitakachowafanya washawishike zaidi na wewe.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji