#SheriaYaLeo (205/366); Weka umakini kwenye maelezo.

Tulipokuwa watoto, tulikuwa tunaweka umakini wetu mkubwa kwenye kila tulichokuwa tunafanya.
Hakutuwa na hali ya kuharakisha ambayo tunayo kwenye utu uzima.
Hata kama ni michezo, tuliweka umakini mkubwa katika kuicheza.
Hilo lilipelekea kuwa rahisi kushawishika kwa sababu umakini wetu ulikuwa mahali pamoja.

Lakini kwenye utu uzima mambo yamebadilika.
Hatuwezi kuweka umakini mkubwa kwenye kitu kimoja.
Badala yake umakini wetu umegawanyika kwenye mambo mbalimbali.
Hilo linafanya isiwe rahisi kushawishika.

Katika mpango wako wa kuwashawishi wengine, ni muhimu kuwarudisha kwenye hali ya utoto kwa kuweza kuweka umakini wao kwenye kitu kimoja na kuacha kuharakisha.

Unapokuwa na wale unaotaka kuwashawishi, waondoe kwenye dunia yak kuharakisha na kutokujali.
Wapeleke kwenye dunia ya kuweka umakini wao kwenye kitu kimoja na kukifuatilia kwa undani.
Kwa njia hiyo itakuwa rahisi kuwashawishi katika yale unayotaka wakubaliane na wewe.

Kwa kuweka umakini kwenye maelezo, unaonekana kujali zaidi na wale unaotaka kuwashawishi hawakushuku kwamba unataka kuwalazimisha chochote.
Hilo linawafanya wawe rahisi zaidi kushawishika.

Sheria ya leo; Maneno ya ushawishi na matendo ya kujionyesha vinaweza kuibua wasiwasi kwa wale unaotaka kuwashawishi; wanaweza kujiuliza kwa nini unatumia nguvu sana kuwashawishi? Kwa kuweka umakini kwenye maelezo na kuwarudisha kwenye dunia yao ya utoto, unakuwa na ushawishi mkubwa kwao bila ya kuibua hali ya wasiwasi.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji