2710; Rahisi kupatikana.

Chochote ambacho ni rahisi kupatikana huwa siyo chenye thamani kubwa na unachohitaji ili kufika kule unakotaka.

Hili ni jambo la msingi kabisa ambalo wengi huwa hawalielewi na kuishia kuwa kikwazo kwao kufanikiwa.

Vitu vyenye thamani kubwa kwenye maisha huwa ni vigumu kupatikana na hilo ndiyo linapelekea wengi kukwama kuvifanya.

Vitu visivyokuwa na thamani huwa ni rahisi kupatikana na hivyo ndivyo vinavyowalevya wengi kwa kujikuta wanahangaika navyo zaidi.

Hata kwenye watu, ambao ni rahisi kuwapata siyo wenye manufaa makubwa kwako.
Kama mtu unaweza kumpata muda wowote bila ya kikwazo basi pia siyo mtu anayeweza kukusaidia kwa mambo makubwa.

Ni watu ambao kuwapata ni shida ndiyo ambao pia wanaweza kukusaidia kupata makubwa unayoyataka.

Wasiojua mtego huu hukimbilia vitu rahisi, wasijue ndiyo vinawavuruga na kuwapoteza kwenye vitu sahihi ambavyo ni vigumu.

Hatua ya kuchukua;
Kila unapoona kitu ni rahisi kupatikana, usifurahie tu kama wanavyofanya wengi.
Badala yake jiulize wapi unakosea, wapi hujachagua kwa usahihi.
Na hapo utajionea wazi wapi hujachagua sawa.

Tafakari;
Vitu rahisi huwa havina manufaa kwa sababu kila mtu anaweza kuvipata.
Vitu vigumu huwa vina manufaa makubwa kwa wababu wengi wanavikwepa.
Nenda walipo wachache na hapo utaweza kufanya makubwa zaidi.

#Let’sBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining