2711; Unachohofia kufanya.
Kile unachohofia kufanya,
Ndiyo hasa unachopaswa kukifanya.
Hofu haimaanishi kitu hakiwezekani,
Bali inamaanisha ni kitu ambacho hujawahi au hujazoea kufanya.
Sasa najua,
Ya kuwa unakumbuka,
Nje ya mazoea yako,
Ndipo penye mafanikio makubwa unayoyataka.
Hivyo basi,
Kile unachohofia kufanya,
Ndiyo unapaswa hasa kufanya,
Kwa kuwa kinakutoa nje ya mazoea yako.
Mtu unayehofia kukutana naye, huyo ndiyo hasa unayemhitaji, hivyo hakikisha unakutana naye.
Yale unayopanga kufanya ila unaahirisha, ndiyo hasa unayopaswa kuyafanya bila kuahirisha.
Watangulizi wetu, waliturithisha tabia, ya kutaka kutunza nguvu zetu kwa ajili ya hatari zinazoweza kutokea muda wowote.
Hivyo hawakuwa tayari kujaribu mambo nje ya mazoea yao.
Lakini kwa sasa mambo yamebadilika, hatari siyo kama za enzi hizo watangulizi wetu wanaishi maporini.
Lakini ile hali ya hofu na wasiwasi bado tunayo.
Tukiweza kuitumia vizuri hali hiyo, lazima tuweze kufanya makubwa.
Hatua ya kuchukua;
Kile unachohofia sana kufanya ndiyo unachopaswa kukifanya.
Tukia hofu kama kiashiria cha usahihi wa kitu cha kufanya.
Inapokuwa rahisi kwako kufanya kitu bila ya hofu yoyote ile, maana yake ni ndani ya mazoea na hapo huna nafasi ya kufanya zaidi.
Toka nje ya mazoea na utapata hofu, hicho ndiyo kipimo cha usahihi wa kufanya.
Tafakari;
Hofu ni kitu ambacho ni sehemu yetu.
Hatuwezi kuondokana nacho kabisa.
Ila tunaweza kukikabili kisiwe kikwazo kwetu.
Na njia bora ya kufanya hivyo ni kufanya kile unachohofia.
Unapohofia kitu, usipokifanya hofu inakuwa na nguvu zaidi.
Lakini unapokifanya hofu hiyo inakosa nguvu na kukimbia.
#Let’sBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining