#SheriaYaLeo (215/366); Tumia hali yao ya ushindani.

Sisi binadamu huwa tuna hali ya ushindani ndani yetu.
Huwa hatupo tayari kuona wengine wanatushinda kwenye kitu fulani, hata kama ni kidogo kiasi gani.

Ili kuwashawishi wengine, tumia hali yao ya ushindani.
Waweke kwenye hali ambayo wanashindana na watu wengine na hawatakubali kushindwa.

Watafanya kila namna ili washinde, ambapo wanakuwa hawajui kama umewatega kwenye hiyo hali ya mashindano ili wafanye kile unachotaka.

Chochote unachotaka watu wafanye, ukiwashindanisha na wengine watakazana kukifanya ili kuwashinda wengine.
Na hapo unakuwa umekamilisha lengo la kuwashawishi.

Sheria ya leo; Unapotaka kuwashawishi watu, mara zote fikiria hili; unawezaje kuwafanya watu waone kile unachowataka wafanye ni wao wenyewe wamechagua kukifanya?
Kuweka hali ya ushindani ni moja ya njia za kuwezesha hilo.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji