#SheriaYaLeo (221/366); Epuka Mabishano.
Mabishano huwa hayana manufaa yoyote.
Hiyo ni kwa sababu kila mtu huwa anaamini maoni yake ni sahihi zaidi.
Hivyo unavyobisha na kupinga maoni ya mtu, humshawishi, bali unamfanya azidi kuamini maoni yake.
Kadiri unavyombishia mtu ndivyo anavyoacha kukusikiliza na kusimamia upande wake.
Kama unataka kuwashawishi watu wabadilike, waonyeshe kwa vitendo na siyo maneno pekee.
Wafanye wao wenyewe waone udhaifu wa maoni wanayosimamia na watashawishika kuyabadili na kusimamia maoni sahihi.
Na hata katika kuonyesha, usiweke moja kwa moja kwamba mtu hayupo sahihi. Badala yake mfanye yeye mwenyewe ndiyo aone kwamba upande aliopo siyo sahihi.
Hilo linawafanya wawe tayari kubadilika wao wenyewe, kwa sababu hawajalazimishwa.
Watu wakiona wanalazimishwa kubadilika, watakataa kufanya hivyo hata kama mabadiliko hayo yana manufaa kwao.
Sheria ya leo; Kuwa makini, usitumie maneno na mabishano kuwasahihisha watu. Badala yake onyesha kwa vitendo na mtu ajionee mwenyewe kwamba upande aliopo siyo sahihi ili awe tayari kubadilika.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji