#SheriaYaLeo (222/366); Waonjeshe dawa yao wenyewe.

Kama ambavyo tumeshaona, mabishano huwa hayafanyi kazi.
Kuwaambia watu kile wanachokosea hakuwafanyi wajirekebishe.
Badala yake watajitetea na kuendelea kukifanya.

Njia bora ya kuwapa funzo ili wabadilike ni kuwaonjesha dawa yao wenyewe.
Hapo unachofanya ni kuwafanyia kile ambacho wamekufanyia wewe, kwa namna ambavyo wamekifanya.

Unakifanya ukihakikisha wanaona wazi umefanya kama ambavyo wao wanafanya.
Hilo linawafanya waone madhara ya kile walichokufanyia.
Kupitia kujifunza kwa vitendo watasukukwa kubadilika.

Kama ambavyo Gracián amewahi kusema, ukweli huwa unaonekana, lakini huwa hausikiki.
Kuwaeleza watu madhara ya kile wanachofanya hawatakuelewa, wataishia kubishana na wewe.
Lakini kuwaonyesha kwa vitendo, kwa kurudia kile ambacho wanafanya, watajionea wenyewe madhara ya kile wanachofanya.

Maneno yanaibua ubishi lakini vitendo vinadhihirisha.
Waonjeshe watu dawa yao wenyewe na watayaelewa madhara ya kile wanachofanya kitu kitakachowasukuma kubadilika.

Sheria ya leo; Kama kuna tabia ambayo unataka wengine waibadili, usihangaike kuwaambia, badala yake waonyeshe kwa vitendo. Rudia tabia hiyo kwao kwa namna ambayo watayaona madhara ya tabia hiyo kwao wenyewe na hilo litawasukuma kubadilika.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji