#SheriaYaLeo (224/366); Bobea sanaa ya maigizo.
Huwezi kufanikiwa kwenye kuwashawishi wengine bila kubobea kwenye lugha na sanaa ya maigizo.
Lazima uweze kupenyeza maneno yenye ushawishi wakati wa mazungumzo na wengine.
Yanakuwa ni maneno ambayo wengine hawayatarajii, lakini yanajenga ushawishi mkubwa kwao.
Ili maneno hayo yawe na nguvu ya ushawishi unapaswa kuyatoa wakati mtu amenaswa kwenye kitu kingine, mfano anafikiria mambo yake mwenyewe au jinsi atakavyojibu kile unachomwambia.
Pale mtu anaposhtukia maneno unayotumia na kuonyesha ni kitu ambacho hakutegemea unaweza kuomba samahani na mkaendelea na mazungumzo ya kawaida.
Mambo mengi duniani ni ya kawaida wakati watu wanapenda zaidi mambo ya kusisimua.
Unapotumia lugha na sanaa ya maigizo katika ushawishi, unawapa watu kitu cha kuwasisimua kitu kinachowafanya wawe rahisi kushawishika.
Unawavutia watu kukufuatilia kwa sababu wanaona una kitu cha tofauti na walivyozoea.
Sheria ya leo; Maigizo ndiyo njia kuu ya kuwashawishi watu. Kutumia lugha yenye mapendekezo na vidokezo mbalimbali wakati wa mazungumzo, inajenga ushawishi kwa watu kitu kinachowafanya wakubaliane na wewe.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji